Indirimbo ya 301 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Njioni tumwimbie Bwana tumfanyie shangwe kuu. Mwamba wa wokovu wetu, tuje kwake na shukrani, tumfanyie shangwe kuu, Bwana ni Mungu mkuu, na Mfalme wa wafalme, tena Bwana wa mabwana.
2
Mikononi mwake zimo bonde zote za dunia. Na vilele vya milima ndiye aliyezifanya, aliifanya bahari na nchi akaiumba, njioni (sic) wote tuabudu, tusujudu Mungu wetu.
3
Tupige magoti yetu mbele ya Muumba wetu. Kwani ndiye Mungu wetu nasi tupo mali yake, na kondoo zake yeye, ingekuwa heri leo, msikie neno lake msifanye mioyo gumu.
4
Kama huko kwa Moria siku za Munga jangwani. Hapo walinijaribu babu zenu hapo kale. Wakanipima kuona matendo yangu makuu, kwa miaka arobaini nikahuzunishwa nao.
5
Nikasema watu hawa waliopotoka mioyo. Hawakuzijua njia zangu niliwaonyesha, nakaapa kwa hasira yangu na kusema hivi: Wasiingie rahani mwangu ya huko Kanaani.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 301 mu Nyimbo za wokovu