Indirimbo ya 102 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sayuni, ulaki Bwanako, umshangilie Mfalme! Jipambe kwa Bwana arusi, ujitengeneze tayari!
Furahi, furahi! Umshangilie Bwanako! Furahi, furahi! Umsujudie Mfalme!
2
Kutoka ‘tukufu wa Baba na kiti cha enzi mbinguni Mwokozi alitufikia kulazwa mtoto horini.
3
Akawa dhabihu kamili, akasulibiwa Golgotha, akafa kwa ‘ajili ya wote, tupewe wokovu wa Mungu.
4
Alitushindia mauti na kumharibu shetani; akaufunua uzima, tupate kuishi milele.
5
Afika kwa wenye huzuni kuwapa faraja na heri, na atamiliki milele, Mfalme wa pendo na haki.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 102 mu Nyimbo za wokovu