Indirimbo ya 235 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tumekombozwa katika nchi, usikilize vema, rafiki!
:/: Tumeokoka tufike juu, taji kutiwa, furaha kuu! :/:
2
Tumekombozwa katika watu, hata tuchekwe kitambo huku.
:/: Twavumilia katika shida, twatazamia ‘heri wa mbingu. :/:
3
Tumekombozwa, tuwe wa huru, tukichokozwa haitudhuru.
:/:Tutaondoka, ‘hamia mbingu, tutasimama mbele ya Mungu.:/:
4
Tumekombozwa, furaha kuu, twaandaliwa karamu kuu!
:/: Salamu hiyo uitangaze, wafike mbio na waokoke! :/:
5
E’ mama, baba, mbona kungoja? Ndugu na dada, fika pamoja!
:/: Mwenye kukawa hataingia, leo waitwa na Yesu pia. :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 235 mu Nyimbo za wokovu