Indirimbo ya 93 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Siku chache, na tena wakristo watakwenda kumwona Mwokozi, siku chache na wataipewa thawabu na taji ya uzima.
Nangoja sana Bwana Yesu kama zamu angojavyo asubuhi. :/: Kwa dalili zote ninaona sasa kwamba Yesu yu karibu ya kurudi:/:
2
Siku chache za vita ya huku, tena Yesu Mfalme atakuja; tutaona furaha na raha, atatupeleka kwake juu.
3
Siku chache machozi ya shida, Mungu atayafuta kabisa. Na baada ya siku si nyingi kwa lango nitaingia mbingu.
4
Baragumu la mwisho ‘talia, waminifu watachukuliwa; wote wataingia mbinguni kukaa pamoja na Mwokozi.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 93 mu Nyimbo za wokovu