Indirimbo ya 32 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Hapo nilikuwa chini Katika dhambi nyingi, roho yangu iliona kufa na giza tele. Mungu alikisikia kilio changu huko, naye akanipandisha, kuniponya.
:/: Nimeokoka, nimeokoka! Yesu Mwokozi wangu aliniokoa:/:
2
Sasa Yesu amekuwa makimbilio yangu, na upendo wake ‘kubwa uko moyoni mwangu. Ne’ma yake kubwa sana inajaliza roho, niwe mwaminifu kwake siku zote!
3
Ewe, mwenye sikitiko, kuna matumaini: Yesu anakufahamu, atakusaidia. Atakupandisha toka tope la kuteleza, upokee ne’ma yake kwa wokovu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 32 mu Nyimbo za wokovu