Indirimbo ya 85 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Twapasha habari ya mbingu, mahali pa watu wa heri, na tunatamani ku’ona ufuko wa nchi ya mbingu.
Sikitiko, wala shida hazitakuwapo mbinguni. Huko juu, huko juu tutashangilia milele.
2
Twapasha habari ya mbingu na mji mzuri ajabu, na jeshi la watakatifu waliomaliza safari.
3
Twapasha habari ya pendo, amani na nguo nyeupe. na raha baada ya vita, makao karibu na Mungu.
4
Twapasha habari ya Yesu, alituokoa na dhambi. Ingawa ni shida njiani atatufikisha mbinguni.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 85 mu Nyimbo za wokovu