Indirimbo ya 290 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Baragumu litalia sana, watu wote watalisikia. Waliokufa watafufuka na wazima watabadilika.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:
2
Na wenye uwezo wa dunia watatetemeka siku ile, na hawataweza kuinuka kutazama uso kama jua.
:/: Nani anayeweza? Yesu, mweza yote. :/:
3
Najua Mchunga wangu mwema, anichunga kwa maisha yangu. Na siku ya mwisho nikishinda, sitaona uchungu wa kufa.
:/:Nani Mchunga mwema? Yesu, mweza yote. :/:
4
Mbinguni hakitafika kitu cha uchafu, dhambi na kuasi. Wasiomwamini Bwana Yesu, gadhabu ya Mungu yawangoja.
:/: Nani atahukumu? Yesu, mweza yote. :/:
5
Mimi Yesu mzabibu kweli, Baba Mungu ndiye mkulima, na ninyi matawi ndani yangu, na hamwezi neno bila mimi.
:/: Nani ni mzabibu? Yesu, mweza yote. :/:
6
Unayempenda Baba Mungu, lazima upende ndugu yako; ukiwa hupendi ndugu yako, huwezi kupenda Baba Mungu.
:/:Nani aliyesema? Yesu, mweza yote. :/:
7
Nawapenda, mwisho wa upendo, na ninyi mpate kupendana; hivyo mataifa wataona ya kwamba m watu wangu kweli.
:/: Nani mwenye upendo? Yesu, mweza yote. :/:
8
Sisi watumishi wake Mungu, tumeacha vyote vya dunia. Tumemchagua Bwana Yesu, tuwekwe kuume kwake Mungu.
:/: Tumshukuru nani? Yesu mweza yote. :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 290 mu Nyimbo za wokovu