Indirimbo ya 251 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Heri mimi kwani Mkombozi wangu alitoa dhambi zote! Shangwe na furaha zanijaza mno, kila siku nafurahi!
Kila siku nafurahi! Kila siku nafurahi! Heri mimi kwani Mkombozi wangu alitoa dhambi zote!
2
Heri mimi, Yesu alinifilia; ni furaha ku’; yu hai! Ni rafiki kweli anayetuweka huru toka minyororo.
Kila siku nafurahi! Kila siku nafurahi! Heri mimi Yesu alinifilia; ni furaha ku’: Yu hai!
3
Heri mimi kwani ananiongoza; nafuata nyayo zake. Nikiyasikia tu maneno yake, sitaweza kupotea.
Kila siku nafurahi! Kila siku nafurahi! Heri mimi kwani ananiongoza, sitaweza kupotea!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 251 mu Nyimbo za wokovu