Indirimbo ya 238 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nifananishwe nawe Mwokozi, ni haja yangu iliyo kuu. Ninakuomba, na kwa machozi, nikufuate, Bwana wa juu!
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye upendo, safi halisi! Unitakase, unijalize! Nifananishwe nawe zaidi!
2
Nifananishwe nawe Mwokozi, mwenye rehema, pendo ajabu! Niwapeleke kwa Mkombozi walioshindwa na majaribu!
3
Nifananishwe nawe Bwanangu, Mtakatifu, mwenye saburi! Niwe mnyofu kazini mwangu, mtu thabiti bila jeuri!
4
Nifananishwe nawe Mwokozi! Nimiminie pendo moyoni! Nibadilishe, e’ Mkombozi, niwe tayari kwenda mbinguni!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 238 mu Nyimbo za wokovu