Indirimbo ya 209 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Uwatafute wanaopotea, na kwa upendo watoe dhambi! Lia pamoja na wenye huzuni, uwapeleke kwa Yesu Mwokozi!
Uwatafute wanaopotea! Yesu Mwokozi awahurumia.
2
Anatafuta waliokimbia, anawangoja warudi upesi. Uwafundishe kwa pendo na kweli ju’ ya neema na haki ya Yesu!
3
Ndani ya roho na katika siri labda waona shauku ya Mungu. Uwaongoze kwa Yesu Mwokozi, wafahamishe upendo wa Mungu!
4
Uwatafute wanaopotea! Mungu atoa upendo na nguvu. Uwapeleke kwa Yesu mpozi, Mwenye huruma na afya kwa wote!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 209 mu Nyimbo za wokovu