Indirimbo ya 55 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tupate kwa nani faraja ya roho? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu. U wapi msingi wakutegemea? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
Kwa Yesu, kwa Yesu ninashangilia kwa roho na moyo. Uheri wa huko haufasiriwi, moyoni wafahamiwa.
2
Na maji mazima yapatwa kwa nani? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu. Na wapi twapata mikate nyikani? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
3
Mahali tutapostarehe ni wapi? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu. Na nguvu ya kuendelea ni wapi? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
4
Ni nani anayebatiza kwa Roho? Ni Yesu, ni Bwana Yesu. Upendo wa ndugu watoka kwa nani? Kwa Yesu, kwa Bwana Yesu.
5
Wakristo watakusanyika kwa nani? Kwa Yesu, kwake mbinguni. Kwa nani watashangilia milele? Kwa Yesu na pendo lake.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 55 mu Nyimbo za wokovu