Indirimbo ya 280 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Jina lake Yesu Kristo linadumu siku zote; jina hili la milele haliwezi kunyauka; linafaa watu wote, na wazee na vijana; linaweza kuongoza kila mtu kwake Mungu.
Jina hili nalipenda, limewasha moyo wangu; na kwa jina hili jema nimepata kuokoka.
2
Jina hili linavuma pande zote za dunia, na kwa wote linaleta tumaini na faraja. Jina hili laondoa uadui na ubaya, hata milki ya Mwokozi itaanza kutawala.
3
Na katika giza huku jina hili linang’aa, laonyesha msafiri njia wazi ya uzima. Jua likitiwa giza, jina hili linadumu; na milele lisifiwe hapa na mbinguni juu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 280 mu Nyimbo za wokovu