Indirimbo ya 278 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ninainua macho yangu kwa Mungu aketiye juu, aliye msaada wangu, njiani pangu nuru kuu. Aliyefanya yote, maombi huyasikia. Katika njia zangu zote atanilinda pote pia.
2
Bwanangu asiache tena mguu wangu usogezwe, kwa kuwa ni mlinzi mwema, naye hatasinzia kamwe. Alinda roho yangu nisije nikapotea. Hitaji za maisha yangu baraka yake ya’enea.
3
Aniokoa na uovu, na roho yangu imepona. Kwa yeye nguvu na wokovu, nilizionja naku’ona. Ananilinda pote: kutoka na kuingia; anijaliza mema yote hata nakutumainia.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 278 mu Nyimbo za wokovu