Indirimbo ya 244 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Safari yangu huku ikiwa hatarini, na ikipita katika giza na jaribu, najua kwa hakika: Mwokozi yu karibu, ninamfuata mahali po pote.
Nikiwa pamoja na Yesu sina hofu. Anipa furaha na heri rohoni mahali pote. Ikiwa nitayashiriki mateso yake, nitamfuata Mwokozi hata mwisho.
2
Nikitangaza neno la Mungu duniani katika mataifa walio wakaidi. Nina furaha kubwa moyoni mwangu, kwani Mwokozi yu nami mahali po pote.
3
Na Bwana akitaka nibaki hapa kwangu, wengine wakitumwa mahali pa ugeni, kusudi langu moja: nidumu mwaminifu, na nimfuate mahali po pote!
4
Si lazima nijue makusudio yote, ni kazi yangu huku kumfuate yeye. Ikiwa nitabaki, ikiwa nitakwenda, nitamfuata Mwokozi po pote.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 244 mu Nyimbo za wokovu