Indirimbo ya 326 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
..Siku kuu ya Mungu imekaribia, mwaliko umetumwa kwako. Mda ni mfupi, tujitayarishe, kwenda kumlaki Bwana Yesu.
Siku inakuja, yawaka kama moto, kimbia hukumu yake Bwana. Siku inakuja, yawaka kama moto, kimbia hukumu yake Bwana.
2
Wewe unasema: ni siku nyingi twaalikwa na wahubiri. Ufahamu kama siku moja kwa Bwana, ni kwama miaka elfu moja.
3
Rafiki ‘jiulize, je umeokoka, kwa matendo na tabia yako? Kama bado, mpendwa, hujui amani, fanya hima uokoke sasa.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 326 mu Nyimbo za wokovu