Indirimbo ya 192 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sauti moja iliniuliza: ” Wajua nilikufanyia nini?
:/: Kwa’jili yako niliteswa sana; ufike kwangu, kwani nakupenda! ” :/:
2
” Nilipokuwa huku duniani wakanitia taji ya miiba,
:/: Na sikupambwa fedha na dhahabu, lakini majeraha na uchungu.” :/:
3
” Golgotha nilifika siku moja, na nilikufa ju’ ya msalaba.
:/: Tazama, katika mikono yangu nimekuchora, e’ mtoto wangu. “:/:
4
Heleluya, rohoni ninaimba! Nimejiweka mikononi mwake.
:/: Na Yesu ananiongoza sasa, nifike nchi nzuri huko juu. :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 192 mu Nyimbo za wokovu