Indirimbo ya 135 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sifu Bwana, ninyi watu wake wote kwa neema yake juu yenu! Yesu Kristo yu karibu, atulinda na’ongoza njia yote.
Sifu Mungu! Sifu Mungu, kwa sababu analinda sisi sote! Sifu Mungu! Sifu Mungu kwa ulinzi wake mwema!
2
Yesu alikusamehe dhambi zote, akuponya udhaifu wako; amekufariji, amefuta chozi, na neema yakutosha.
3
Anakutilia afya, nguvu mpya, akuvika vazi la kushinda. Katika mapito yake waongozwa na kulindwa kwa salama.
4
Kaa ndani yake Bwana Yesu Kristo, haki yetu, utakaso wetu, na wokovu, na hikima vile-vile, Mkombozi ‘timilifu.
5
Bwana Yesu atakuja siku moja, atukaribishe wote kwake. Tutamtukuza yeye, Bwana wetu, kwani alitukumboa.
Uje mbio! Uje mbio! Bwana Yesu utukaribishe kwako! Uje mbio! Uje mbio! Tunaomba wote: Uje!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 135 mu Nyimbo za wokovu