Indirimbo ya 347 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Oh mara ngapi tunasumbuka na roho inalegea, tunazungukwa na giza kubwa tunaogopa sana. Sauti tamu ya Bwana yesu tunasikia kusema, mtoto wangu ninakupenda, sitakuacha daima.
Kwa kila wakatiii, kwa kila pahali Aliahidi kuchunga, hataniacha daima. Kwa kila wakatiii, kwa kila pahali, Aliahidi kuchunga, hataniacha daima.
2
Mpenzi umesahau mbio sauti hii ya mapendo, ya Bwana Yesu aliyetoa uzima wake kwako. Mtoto unayechoka sana kumbuka sitakuacha, niliahidi nitakuchunga na kuwa nawe daima.
3
Halafu ndugu ufarijiwe katika kila matata, Mwokozi wako anakupenda na kuikaa nawewe. Nyoosha kwake mkono wako utamkuta karibu, Faraja tamu kumusikia sitakuacha daima.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 347 mu Nyimbo za wokovu