Indirimbo ya 185 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Neema kubwa ya Mungu wetu: Alikutuma kwa kazi yake kwenda kuzipanda mbegu njema katika roho za wenzako!
Nenda, E’ mvunaji, nenda, e’mvunaji! Nenda kapande mbegu njema, nenda, e’mvunaji!
2
Njia ikionekana ndefu, neno la Mungu ni aminifu: “Kwa macho yangu nakuongoza, jangwani nitafanya njia”.
3
Ikiwa ndugu hawakuoni, mtumikie Mwokozi vema! Bwana anayetazama wewe, anampenda mwaminifu.
4
Hata ukiwa mdogo sana, nenda upesi shambani mwake, labda utaliokota suke lililoachwa na wenzako.
5
Neno na nyimbo hazitatosha kuwaamsha wafanya dhambi, bali mwenendo ulio safi utawavuta ndugu zako.
6
Na usichoke kupanda mbegu katika pendo na tumaini! Ukizipanda kwa shida nyingi, kwa shangwe kubwa utavuna!
7
Siku za kazi zita’pokwisha tutahamia mbinguni juu; tutawaona wenzetu wote tuliovuta kwa Mwokozi.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 185 mu Nyimbo za wokovu