Indirimbo ya 160 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Ahadi zote za Mungu wetu zinasimama hata milele. Milima yote ikianguka, ahadi hazipunguki.
Ahadi zake zinasimama, hazipinduki hata milele. Ikiwa nyota zingezimika, ahadi zake zinadumu.
2
Ahadi zake zinasimama katika shida, katika giza. Na nikichoka kwa vita kali, ahadi hazipunguki.
3
Ahadi zake zinasimama katika homa, katika kufa. Nafarijiwa na Baba yangu, ahadi hazipunguki.
4
Ahadi zake zinasimama; nitaamshwa katika kufa. Kwa Baba nitapokea taji; ahadi hazipunguki.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 160 mu Nyimbo za wokovu