Indirimbo ya 166 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tukienda pamoja, tukishikamana na Mungu, tunapata amani na raha; tukifanya daima yanayompendeza, yu karibu kutusaidia.
Raha, furaha twazipata kwa Yesu, tukidumu katika kuamini, kutii.
2
Ikiwapo dhoruba, na mawimbi ya’vuma, yanakoma kwa neno la Yesu. Tukiona jaribu na kuhofu adui, tutashinda kwa nguvu ya Yesu.
3
Tukibeba mizigo anatustarehesha, tunapata furaha halisi. Masumbuko yatoka, giza inageuka kuwa nuru njiani mwa Mungu.
4
Tuna raha ya Mungu katika mashindano tukitii na tukiamini. Jua lake la pendo linawaangazia watiio na waaminio.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 166 mu Nyimbo za wokovu