Indirimbo ya 74 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mgeni mimi mahali pa ugeni, na kwenda mbali mno katika nchi nzuri. Na ni mjumbe huku kutoka Mungu wetu, nina habari ya Mfalme.
Habari yake nzuri sana, furaha yao malaika: «Mpatanishwe sasa na Mungu Baba yetu»! Habari yake ndio hiyo.
2
Salamu ya Mwokozi kwa kila mtu hapa: Urudi kwake Mungu, utoke utumwani! Ufike kwake Yesu, tubia dhambi zako! Habari hiyo ya Mfalme!
3
Mbinguni nchi nzuri, yapita vitu vyote, furaha huko tele na raha ya milele. Ukiamini Yesu uta’pokea huko. Habari hiyo ya Mfalme!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 74 mu Nyimbo za wokovu