Indirimbo ya 258 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mkutano ‘kubwa gani mlimani mwa Sayuni asubuhi ya milele? Hawa walinunuliwa tena walitakasiwa, wawe malimbuko kwa Mwokozi.
2
Hata kufa huku chini walikuwa waamini, walimfuata Yesu. Sasa wanaka’ mbinguni, wametoka jaribuni, wamerithi raha yakipeo.
3
Ukamili wa uzuri wa muziki na zaburi unatoka huko juu! Ni sauti tamu mno ya kinubi na ya wimbo kandokando ya Mwokozi wetu!
4
Wimbo huo ni wa nani, wa sauti ya tufani, wa kutia raha kuu? Ndio wimbo mpya ule uimbwao sasa kule ili kuhimidi Mkombozi.
5
Bwana, unilinganishe, na ulimi u’safishe, nami nikaimbe huko! Nipe vazi la rohoni, safi sana, la kitani lifaalo asubuhi hiyo!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 258 mu Nyimbo za wokovu