Indirimbo ya 5 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Dhahabu na fedha haziniokoi, Hazina na mali haziponyi roho, Lakini kwa damu ya Yesu Mwokozi Nime nunuliwa nipate uhuru.
Nakombolewa pasipo mali, kwa neema nimeokoka! Ni bei ghali: kwa damu yake alilipa deni langu.
2
Dhahabu na fedha hazinilipii madeni makubwa ninayo kwa Mungu. Mwokozi alinikomboa kwa damu. Nipate wokovu nitoke dhambini.
3
Dhahabu na fedha haziufungui Mlango waku’karibia Mwokozi, Lakini kwa damu nimeifikia Neema ya Mungu aliye mkuu.
4
Dhahabu na fedha hazinifikishi Nyumbani mwa Mungu nilie mwasia, Lakini nimekombolewa kwa damu, Kwa hiyo nitachukuliwa mbinguni.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 5 mu Nyimbo za wokovu