Indirimbo ya 113 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Msalabani Mwokozi wangu alijitoa kuniokoa, na damu yake ilimwagika kwa’jili yangu, kunikomboa.
E’ Golgotha, e’ Golgotha, alipoteswa Bwana Yesu! E’ Golgotha, e’ Golgotha, nilipopata raha kweli!
2
Na nchi ile ilitetema, mbinguni jua likafunikwa wakati Yesu alipokufa, akichukua hatia yangu.
3
Likapasuka pazia lote, kwa hiyo neno limetimizwa. Naona njia ya mbingu wazi: Nikutakaswa kwa damu yake.
4
Mwokozi wangu, upendo gani: Uliutoa uzima wako! Kunikomboa ulisikia mateso yote ya msalaba.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 113 mu Nyimbo za wokovu