Indirimbo ya 195 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tunasikia leo habari, inawaita watu wafike; watu wa hapa, watu wa mbali, wote wapate sasa wokovu!
2
Mtu wa dhambi uje upesi, Yesu angoja kukuokoa! Tena kwa nini unachelewa? Leo ni siku ya kuokoka.
3
Ulikimbia Yesu Mwokozi aliyekukomboa kwa damu. Usikimbie mbali zaidi, ila urudi, uje upesi!
4
Katika dhambi hutaiona raha halisi, hata kidogo. Yesu mwenyewe atakujaza raha ya kweli ndani ya roho.
5
Mtu wa heri katika shida, katika mambo yote ya huku, ni hali ya mkristo wa kweli, mtu wa heri hata milele.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 195 mu Nyimbo za wokovu