Indirimbo ya 277 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nitaogopa nini gizani duniani? Sikuachiwa peke’ mbali ya tumaini! Mwokozi yu karibu, asiyebadilika.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:
Namshukuru Mungu asiyebadilika. Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika.
2
“E’ usifadhaike moyoni mwako, mwana”, anong’oneza Yesu, “Nitegemee sana!” Na hapo woga wangu waruka kwa hakika.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:
3
Na nikijaribiwa na jua lifichwapo, hata sioni raha, wala faraja hapo, nakimbilia Yesu, na yote yapinduka.
:/: Hutunza ndege ndogo na mimi kadhalika:/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 277 mu Nyimbo za wokovu