Indirimbo ya 237 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwokozi wangu ni mwamba bora, ahadi kama milima; zaniletea amani tele, na mibaraka daima. Katika mwamba ni raha kuu, baraka tele kutoka juu. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.
2
Makimbilio ni mwamba huo katika teso lo lote; Nisikimbie adui ‘kuu, nishinde katika vyote! Dunia yote ikitingika, ahadi zake hazipunguki. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.
3
Nakaa mbali ya udhalimu, hatia, dhambi, hukumu. Na kwa imani nikisimama, adui atakimbia. Nayo mawazo ya giza tupu hayatapata nafasi huko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.
4
Nafurahia baraka zote za ulimwengu wa roho. Karama hizo nalizipewa katika kufa kwa Yesu. Hakuna woga na shaka huko, hayatakuwa manung’uniko. Nakaa humo, ninastarehe, ni heri sana milele.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 237 mu Nyimbo za wokovu