Indirimbo ya 141 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwokozi wetu anatupa furaha duniani, atuongoza kwa neema na anatushibisha. Tazama, yupo pamoja nasi, neema haitaisha kamwe! Haleluya, haleluya, haleluya, Amina!
2
Ni vema kumpenda Mungu aliyetukomboa, vizuri kuwa mtu wake, sitapotea kamwe. Furaha yetu itabakia, ikiwa vyote vingetoweka. Haleluya, haleluya, haleluya, Aminia!
3
Ikiwa giza mara nyingi, na jua likifichwa, na tukijaribiwa huku twajuwa ni kwa mda. Mbinguni hatutaona kamwe huzuni wala machozi tena. Haleluya, haleluya, haleluya, Aminia!
4
Na tusisumbukie tena chakula wala nyumba, maana vyote twavipata kwa ne’ma yake Mungu. Njiani yote atuongoza aichukuwa mizingo yetu. Haleluya, haleluya, haleluya, Aminia!
5
Ikiwa vema huku chini kutegemea Yesu, furaha gani huko juu kuona uso wake. Tutaiona furaha tele, na utukufu hautaisha, Haleluya, haleluya, haleluya, Aminia!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 141 mu Nyimbo za wokovu