Indirimbo ya 79 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Maisha ya mtu [mafupi] ya hapa dunia yanaifanana safari chomboni. Twapita bahari katika hatari, lakini Mwokozi anatuongoza.
Ikiwa Mwokozi anatuongoza twaweza kuona amani na raha, atatufikisha salama mbinguni, na humo hatutakumbuka safari.
2
Twapita katika baridi na pepo, maneno ya Mungu ni nuri gizani. Hatari na hofu na chombo kibaya hatuta’kumbuka karibu na Yesu.
3
Ingawa mawimbi yapiga kwa nguvu, tunakaribia bandari upesi. Na humo hakuna dhoruba na pepo; safari tutaimaliza salama.
4
Tutakapofika bandari ya mbingu tutamshukuru Mwokozi mkuu. Hatutaziona hatari na hofu karibu na Yesu mwenyewe mbinguni.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 79 mu Nyimbo za wokovu