Indirimbo ya 270 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Simama, fanya vita pamoja na Mfalme! Bendera tuishike iliyo ya Mwokozi! Mwenyezi huongoza majeshi yake huku. Adui wote pia washindwa mbele yake.
2
Sikia baragumu, linatuita sasa! Tuendelee mbele, kusudi ni kushinda! Tusiogope kamwe hatari ya shindano, pigana na adui kwa nguvu yake Mungu!
3
Sima, fanya vita kwa jina lake Yesu! Hatuna nguvu sisi, tunamtegemea. Na kwanza tuzivae silaha zake Mungu! Tukeshe siku zote, tuombe kwa bidii!
4
Shindano letu hapa ‘takwisha siku moja; twapiga vita leo, baada pumziko. Na kila mshindaji atapokea taji, na utukufu tele karibu na Mfalme.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 270 mu Nyimbo za wokovu