Indirimbo ya 122 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwokozi kamili ni Yesu pekee, Mwokozi mzuri halisi. Katika wokovu wa Mungu mkuu ninalindwa naye kabisa.
Katika wokovu nalindwa salama, naishi kwa maji ya ‘hai. Upendo wa Mungu unanizunguuka :/: na kanihifadhi daima. :/:
2
Baraka ya mbingu inanijaliza kwa Roho ya utakatifu. Nasifu Mwokozi katika furaha, wokovu umenifikia.
3
Mwokozi mzuri ni Yesu pekee, aniondoaye mizigo. Njiani ananiongoza vizuri, anipa na nguvu ya mwendo.
4
Nitakapomwona Mwokozi mbinguni baada ya shida za huku, Nitamhimidi na kumshukuru Bwana ninayempenda.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 122 mu Nyimbo za wokovu