Indirimbo ya 35 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nimefika kwake Yesu, Na rohoni mwangu sasa, jua lake la neema linang’aa kila siku.
Roho yangu inaimba, nimefunguliwa kweli. Nimekaribia Yesu, ninaimba kwa furaha.
2
Pepo za neema yake zinavuma ndani yangu, na mawimbi ya wokovu yananijaliza sasa.
3
Sasa Bwana Yesu Kristo amefanya kao kwangu. Nimepewa mfariji, Roho ya ahadi yake.
4
«Siku roho afikapo mtajua kwa hakika kwamba ninakaa kwenu», hivyo Yesu alisema.
5
Kweli, amefika kwetu, sasa yumo ndani yetu. Ujitoe kwake Mungu, aioshe roho yako!
6
Yesu atakapokuja katita utakatifu, nitafananishwa naye, nitamshukuru sana.
Zitakuwa nyimbo nyingi tuta’poingia mbingu, na milele tutaimba na kusifu Mungu wetu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 35 mu Nyimbo za wokovu