Indirimbo ya 287 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tunamtia mikononi mwako mtoto huyu, umtunze sana, na kila siku kwa neema yako umbariki, Bwana Yesu Kristo!
2
Ulimwengu kuna majaribu mahali pote, shida na mitego. Lakini uwe mchungaji wake, na umwongoze, E’ rafiki mwema!
3
Mwokozi kwa upendo ‘mchukue, asije akashindwa safarini! Na umlinde kwa rehema yako, apate kuwa wako siku zote!
4
Utume nuru ya neema kwake na maji ya uzima toka kwako e Bwana Yesu. Twakuomba leo ulinde mwana wetu kwa salama.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 287 mu Nyimbo za wokovu