Indirimbo ya 234 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Utukufu wa mbinguni ni wa heri na amani, dhambi hazitakuwamo. Vitu vyote vilivyomo ni vya tunu na thamani, dhambi hazitakuwamo.
Dhambi hazitaingia mbingu ya utakatifu. Ukidumu mwenye dhambi bila kutakaswa huku, hutaingia mbinguni.
2
Kama unatumaini kufikia nchi ile na kuona Bwana Yesu, utafute utakaso na kupata moyo safi! Dhambi hazitakuwamo.
3
Unaweza ‘tenda dhambi na kukana Bwana Yesu, walakini ukumbuke: Dhambi zako zitafunga lango la mbinguni, kwani dhambi hazitakuwamo.
4
Na ukiwa mkaidi hata sa’ ya kufa kwako, utaitwa hukumuni, na utaambiwa huko: “Ondokeni siwajui!” Dhambi hazitakuwamo.
Ukitaka kufikako mbingu ya utakatifu, tubu sasa, hacha dhambi, utafute moyo safi, na utaingia mbingu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 234 mu Nyimbo za wokovu