Indirimbo ya 307 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Walikombolewa waimba juu, wakisujudu mbele zake Bwana. Huzuni na taabu zake dunia Bwana amewaondolea zote.
Wanamwimbia Mwana Kondoo aliyekufa, sasa yu hai, ameyashinda mauti.
2
Wanashika vinubi mikononi wakiimba wimbo wa Mwana Kondoo na Musa mtumishi wake Mungu, wakifurahia kushinda kwake.
3
Wasiopenda kumsujudia, katika dunia hii ya sasa. Hawataonekana mbele zake, watateketea motoni kweli.
4
Mda unaobaki ni mfupi, tujitayarisheni ndugu sasa. Bwana ajapo tuwepo tayari, tutaimba naye kule mbinguni.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 307 mu Nyimbo za wokovu