Indirimbo ya 183 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Panda mbegu njema, anza asubuhi, na uwaokoe watu wa shetani! Kwa wakati wake vuno litaivya, chumo utapata kwa furaha kuu.
:/: Twende tukavune, twende tukavune, kwa furaha kubwa twende tukavune! :/:
2
Panda mbegu njema juu ya milima! Na tuendelee hata mabondeni! Neno lake Mungu litawafungua watu wa gizani, kwa furaha kuu.
3
Panda mbegu njema hata kwa machozi, ukumbuke Yesu, leo uhubiri! Bwana wetu, Yesu, atakuja tena na thawabu yetu kwa furaha kuu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 183 mu Nyimbo za wokovu