Indirimbo ya 184 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nitakwenda mahali pa giza na dhambi kuhubiri Injili ya nuru, ili watu wasiosikia habari wafahamu upendo wa Yesu.
Nitakwenda mahali pa giza na dhambi, hata wote wapate kuona wokovu.
2
Akitaka niende kwa watu wagumu na kuacha rafiki na ndugu, hata wakinitaja: ” ‘pumbavu ” na “bure”, nachagua mapenzi ya Yesu.
3
Uliyezipoteza dakika na saa kwa tamaa ya mambo ya huku, uamke na uwaokoe wenzako, hata wasipotee kwa dhambi!
4
Watu wengi wangali watumwa gizani, wanangoja kupata uhuru, Yesu ananituma, niende upesi kuhubiri maneno ya nuru.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 184 mu Nyimbo za wokovu