Indirimbo ya 177 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi, sifa iliyotangazwa na malaika zamani: Mungu wa ju’ atukuzwe, iwe amani duniani!
Nipe habari ya Yesu, uiandike rohoni! Uniimbie zaburi ya kumsifu Mwokozi!
2
Nipe habari ya Yesu, jinsi alivyohimili shida, jaribu na teso na umaskini na bezo (sic)! Maradhi zangu (sic) na dhambi aka’chukuwa mwenyewe, kila wakati tayari kusaidia wahitaji.
3
Nipe habari ya Yesu, ya msalaba na kufa, taja kaburi mwambani, alipotoka Mwokozi! Pendo la Yesu ni kubwa, aliyekufa Golgotha, akafufuka hakika, namshukuru siku zote!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 177 mu Nyimbo za wokovu