Indirimbo ya 259 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Nafikiri siku tutakayofika mbinguni huko kwetu, na malaika kwa furaha watatukaribisha.
Wataimba wimbo wakutupokea: “Karibuni! Karibuni wote kwetu!” Malaika wa Mungu watatulaki kwa nyimbo za furaha: “Twawasalimu! Karibu kwetu!”
2
Mkutano ‘kubwa umekwenda mbele na sasa uko kule. Huimba kwa sauti kuu ukimsifu Mungu.
3
Sisi nasi tutakusanyika huko Yerusalemu mpya, na mkutano wa wakristo utatuamkia.
4
Bwana Yesu naye atatupokea, atatukumbatia katika nyumba ya mbinguni iliyo ya milele.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 259 mu Nyimbo za wokovu