Indirimbo ya 202 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Njoo kwa Yesu Mwokozi, unayeteswa rohoni! Damu iliyomwagika itakuosha kabisa.
Njoo kwa Yesu Mwokozi, naye atakuokoa! Ulimwenguni ni dhiki, kwake ni raha halisi.
2
Mbona kukawa dhambini bila uzima wa Mungu? Uje upesi kwa Yesu ili upate amani!
3
Saa zapita upesi, hazitarudi kabisa. Bado kidogo na tena utapelekwa kuzimu.
4
Yesu atamchukua bibi-arusi mbinguni, na tutaimba milele sifa za Mwana-kondoo.
Huko karibu na Yesu, mbali ya mambo ya nchi, huru na heri rohoni nitafurahi milele!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 202 mu Nyimbo za wokovu