Indirimbo ya 327 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Katika giza la usiku, pakawa na kelele kuu. Tazama Bwana yu karibu, tokeni mwende kumlaki.
:/: Tazama, Bwana yu karibu, Tokeni mwende kumlaki. :/:
2
Na wanawali wote kumi, wakachukua taa zao. Lakini tano wapumbavu wapungukiwa na mafuta.
3
Wakawasihi wa busara, tupeni kwa mafuta yenu. Zinazimika taa zetu, na hatujui tutendalo.
4
Wakawajibu wa busara, hayatutoshi sisi nanyi. Mwendeni kwao wauzao mkajinunulie sasa.
5
Na wakaenda kununua, akaja Bwana wa arusi. Watano walio tayari wakaingia arusini.
6
Mlango hapo ukafungwa, halafu wale wapumbavu wakaja nao, wakalia, tufungulie, Bwana wetu.
7
Bwana arusi akajibu: amina, siwajui ninyi. Kesheni basi, kwa sababu hamjui siku yangu.
:/: Tazama, Bwana yu karibu. Jitayarishe kumlaki.:/:
8
Gizani, nje ya arusi, wakasimama wapumbavu. Kulia wakalia sana, tufungulie, Bwana wetu.
:/: Na jibu likatoka wazi: Mmechelewa kuingia. :/:



Uri kuririmba: Indirimbo ya 327 mu Nyimbo za wokovu