Indirimbo ya 313 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Kumbe wakati wapita mbio, ni sawa jana mlipofika, mlitumika pamoja nasi, na sisi wote tulifurahi.
2
Na kazi yenu tuliipenda, hamkuchoka kutufurahisha. Taabu yenu haiko bure, ni Bwana Yesu atawalipa.
3
Mnaporudi mlikotoka twaomba Mungu mrudi tena. Kutumika pamoja nasi, kazi ni nyingi zinazowangoja.
4
Machozi mengi yalengalenga kwa macho yetu mnapotuacha, ni siku gani tutaonana. Mwenyezi Mungu ndiye ajua.
5
Salamu sana kwa nchi yenu, kwa makanisa na wakristo, sema Mwokozi ni Yesu peke, aliyekwisha kutusamehe.
6
Pasha habari ya ile hati ya mashitaki imetundikwa na imekazwa kwa nguvu sana, msalabani ifedheheke.
7
Na ile hati ya adui, ni Bwana Yesu ameifuta, hakuna tena hukumu kwetu tunaokaa ndani ya Yesu.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 313 mu Nyimbo za wokovu