Indirimbo ya 106 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Tuimbe asubuhi hii juu ya siku manabii walioitabiri! Ni siku kubwa, siku nzuri, upendo umedhihirika, upendo wake Mungu. Sisi sote tufurahi, tumwimbie na kusifu Yesu, Mwokozi wetu!
2
Yu sura yake Mungu Baba, lakini mtu, ili sisi tupate kumjua. Yuaja na amani kwetu, Kuwatafuta wapotevu na kuwaponya wote. Sisi sote tuungane naye Yesu na tupate pendo na uzima wake!
3
Ataliona sikitiko, na kufahamu shida yetu asaidie sisi! Atafundisha haki kweli, kweli, Nakutufahamisha pendo katika kufa kwake, sisi sote tuokoke, na tufufuliwe naye, mbingu zitufunguliwe!
4
Aliye jua la neema afika na wokovu kwetu, na atuangazia. Mchunga wetu yupo nasi, anakutaka tuwe wake, tumfuate kweli! Sisi wake tumjue, tuingie kwake juu, tufanane naye Yesu!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 106 mu Nyimbo za wokovu