Indirimbo ya 7 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Mwokozi ameutimiza wokovu Kwa neema kubwa, na juu ya mwamba wa neno la Mungu najenga imani.
Aliniokoa kabisa. Kwa damu alinisafisha. Ninamshukuru Mwokozi kwa sababu alinikomboa hakika!
2
Mzigo wa dhambi aliuondoa kwa neema kubwa. Naona furaha rohoni kabisa, Amani yangu.
3
Naweza kukaa mweupe rohoni kwa neema kubwa; na Roho ya Mungu inaniongoza njiani daima.
4
Karibu na Yesu nalindwa salama kwa neema kubwa. Ahadi za Mungu zanipa furaha iliyo kamili.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 7 mu Nyimbo za wokovu