Indirimbo ya 200 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Njoni wote, mle, mnywe, Yesu anasema hivyo. “Nimetoa mwili wangu kwa ajili yenu ninyi.” Kila mtu mwenye njaa aje na apate kula! Na aliye na makosa atasamehewa yote.
2
Ninakuja kwako, Yesu, unithibitishe moyo! Uliona umaskini, niwe mwenye uta-jiri. Nishibishe mema yako na karama takatifu! Unijaze Roho yako kama ulivyoahidi!
3
Yesu, ninakuja kwako niungane nawe, Bwana! Mimi mwenye udhaifu, nakutegemea wewe. Na kwa damu yako, Yesu, ninatakasika sasa. Nashiriki mwili wako katika agano jipya.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 200 mu Nyimbo za wokovu