Indirimbo ya 261 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Msafiri uliye njiani, watamani nyumba ya babako. Sikiliza nyimbo za mbinguni! U karibu sana kufikako.
Utakuwako huko, katika mkutano wa wakristo huko mbinguni kwa raha ipitayo fahamu? Utakuako huko wakati wa kuimba wimbo mpya wa kumsifu Mwokozi siku zote?
2
Sikiliza sasa makengele yapigwayo huko juu kwetu, ili kutuita sisi mbele ya jioni ya maisha yetu!
3
Labda siku ile ni karibu nitakapokwenda, nitahama! Sitaona tena majaribu, nitajazwa kwa kumtazama.
4
Lango la mbinguni wazi sasa, Yesu amelifungua kwako. Utaweza kuokoka hasa, usiharibishe heri yako!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 261 mu Nyimbo za wokovu