Indirimbo ya 173 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Maisha katika dunia ni kama kupanda na ‘vuna: Apandaye katika mwili atavuna uharibifu; tukitumikia Mwokozi tutapata thawabu mbinguni; yafaa kuishi na kufa katika maneno ya Mungu.
2
Kwa neema kubwa kabisa tumekubaliwa na Mungu, kwa neema kubwa zaidi twapata kumtumikia. Kuishi kwa ‘jili ya Yesu kati’ yote ya dunia hii na kuitangaza injili ni faida kwetu kabisa.
3
Wakristo wata’poingia mbinguni kusifu Mwokozi, na mimi nataka kufika kuimba pamoja na wao. Tutamshukuru Mwokozi aliyetununua kwa damu; waliohudumu kwa pendo watamhimidi milele!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 173 mu Nyimbo za wokovu