Indirimbo ya 212 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sauti ya Yesu niliisikia, kwa pendo aliniambia: “Ufike, nataka kukusaidia, nangoja, nangoja, ufike!”
Njoo kwa Yesu, ufike upesi, uupokee wokofu wa Mungu! Mbona kukawa dhambini, rafiki? Yesu anakuita, njoo!
2
Ukiwa na hofu kufika kwa Yesu, uliye na dhambi rohoni, kumbuka ya kuwa huruma ni tele; ufike kwa Yesu, angoja!
3
Ukiwa maskini, dhaifu kabisa, Mwokozi anakufahamu. Anakuambia: ” Pokea neema, uache mzigo wa dhambi!”
4
Na kama nilivyo ninamfikia Mwokozi aliyenipenda. Ninaupokea wokovu na raha; kwa shangwe ninamshukuru!



Uri kuririmba: Indirimbo ya 212 mu Nyimbo za wokovu