Indirimbo ya 138 mu NYIMBO ZA WOKOVU

1
Sasa tayari kwetu siku ya kuokoka, Yesu alitimiza yote msalabani. Wengi wanamjia Yesu Mwokozi wao, wapate kustarehe, wapone nafsi zao.
Mwana-kondo’ wa Mungu tunakusifu sana! Uzima uliweka kwa’jili yetu sisi. Umetufanya kuwa mitume yake Mungu. Kati’ majina yote lako ni kubwa mno.
2
Wewe kwa damu yako ulikomboa sisi, na jua la neema linatuangazia. Tumefahamu sasa pendo la Mungu wetu. Damu imetuunga kati’ agano jipya.
3
Njoo upesi nawe uliyesitasita! Mungu atakujaza neema yake kubwa, raha rohoni mwako inayokutuliza, matumaini, nguvu, pendo lililo bora.



Uri kuririmba: Indirimbo ya 138 mu Nyimbo za wokovu